8 Aprili 2015 - 13:35
Hali ya amani Yemen yazidi kuwa mbaya

Shirika la msalaba mwekundu limeonya hali ni ya maangamizi katika mji wa kusini mwa Yemen wa Aden huku majeshi yanayomuunga mkono Rais aliyetoroka Yemen Abedrabbo Mansour Hadi yakishirikiana na magaidi wa Al-qaida na Daesh yakipambana na wanaharakati wa shia wa Huthi katika mji huo.

Shirika la msalaba mwekundu limeonya hali ni ya maangamizi katika mji wa kusini mwa Yemen wa Aden huku majeshi yanayomuunga mkono Rais aliyetoroka Yemen Abedrabbo Mansour Hadi yakishirikiana na magaidi wa Al-qaida na Daesh yakipambana na wanaharakati wa shia wa Huthi katika mji huo.

Wanaharakati wa shia wa kundi Huthi wamejaribu kueneza mashambulizi yao katika eneo la Muallah mjini Aden wakipania kuudhibiti mji huo lakini wamekabiliwa na mashambulizi makali kutoka kwa wanajeshi na wapiganaji wanaomuunga mkono Rais wa Yemen aliyetorokea Saudi Arabia Abedrabbo Mansour Hadi.

Walioshuhudia mapigano hayo wamesema majeshi ya majini ya Saudi Arabia ambayo inaongoza kampeni ya mashambulizi ya angani dhidi ya Wananchi wanaompinga rais na wana harakati wa shia wa kundi Huthi kwa wiki mbili sasa, yameyashambulia maeneo ya wana harakati hao wa kishia mjini Aden lakini muungano huo wa nchi za kiarabu na za ghuba umekanusha kufanya operesheni kwa kutumia majeshi ya majini, kwani wanahofia kuambiwa wanawasaidia magaidi wa Al-qaida na Daesh ambao wameelemewa na kurudishwa nyumba mpaka fukwe za baharini

Hali ni ngumu mno kote Yemen

Msemaji wa shirika la kimataifa la msalaba mwekundu Marie Claire Feghali amesema hali ni ngumu mno kote nchini Yemen kutokana na Saudia arabia kufanya mashambulizi ya angani, majini na ya nchi kavu ambayo yamekatisha njia zote za kuwasilisha misaada ya kibinadamu inayohitajika kwa dharura.

Hata hivyo Jenerali Ahmed Assiri wa Saudi Arabia anayeongoza kampeni ya kijeshi amekanusha madai hayo ya shirika la msalaba mwekundu na kusema maeneo mengi mjini Aden yako salama. Shirika la kimataifa la madaktari wasio na mipaka la MSF limesema hali inazidi kuwa mbaya kila uchao.

Assiri amesema kibali kimetolewa kwa misaada ya vifaa na wahudumu wa matibabu kufikishwa nchini humo kutoka Djibouti na shirika la msalaba mwekundu limesema linatumai kuwasiliha tani 16 za misaada ya vifaa vya matibabu mjini Sanaa hii leo kwa ndege kutoka Jordan.

Shirika la afya duniani limesema zaidi ya watu 560 wameuwa nchini Yemen, katika kipindi cha wiki mbili zilizopita wengine zaidi ya 1,700 wamejeruhiwa na maelfu kuachwa bila ya makaazi huku umoja wa Mataifa ukisema unahofia idadi ya waathiriwa ni kubwa hata kuliko hiyo.

Marekani kuisaidia Saudia arabia kushambulia Yemen

Waziri wa Ulinzi wa Marekani Ashton Carter ametangaza kuwa wanaharakisha kutuma silaha kuunga mkono kampeni ya kijeshi inayoongozwa na Saudi Arabia huku akionya kuwa wanamgambo wenye itikadi kali wa mtandao wa kigaidi wa Al Qaeda huenda wakachukua fursa ya kuwepo msukosuko Yemen kueneza ngome zao nchini humo.

Nchi za kiarabu pia zinalitaka baraza la usalama la Umoja wa Mataifa kuwaweka katika orodha ya watu wa kuwekewa vikwazo mwana wa kiume wa Rais wa zamani wa Yemen Ahmed Saleh na kiongozi wa Wanaharakati wa shia wa kundi Huthi Abdulmalik Houthi.

Waziri wa mambo ya nje wa Iran Javad Zarif ambaye nchi yake inaunga mkono wananchi wa Yemen na inapinga vikali mashambulizi yanayofanywa na Saudia arabia na Marekani dhidhi ya raia madhulumu wa Yemen anatarajiwa kufanya mazungumzo hii leo na viongozi wa Pakistan mjini Islamabad kuhusu hali hiyo ya Yemen.